Jumatatu , 6th Jun , 2016

Chama cha kutetea watumishi wa hifadhi,majumbani,watoa huduma na wa kwenye Mahoteli nchini Tanzania CHODAWU kimeitaka wizara ya mambo ya ndani kuwachukulia hatua wamiliki wa hoteli wanaokiuka sheria ya uajiri wa wafanyakazi wageni.

Chama cha kutetea watumishi wa hifadhi,majumbani,watoa huduma na wa kwenye Mahoteli nchini Tanzania CHODAWU kimeitaka wizara ya mambo ya ndani kuwachukulia hatua wamiliki wa hoteli wanaokiuka sheria ya uajiri wa wafanyakazi wageni kwani kumekuwa na ongezeko kubwa la wageni wanaofanyakazi nchini kinyume na sheria.

Akiongea na East Africa Radio katibu mkuu wa CHODAWU Mkoa wa Kinondoni John Msele amesema kuwa sheria inamtaka mwekezaji kuajiri watumishi wasiozidi watano toka nje ya nchi tena wawe ni wenye uwezo ambao watanzania hawawezi kufanya ili waweze kujifunza lakini katika sehemu nyingi za kazi kuna idadi kubwa ya wafanyakazi toka nje ya nchi.

Akitolea mfano katika sekta ya utalii nchini Bw Msele amesema kuwa kwenye mahoteli mengi makubwa kunaidadi kubwa ya wafanyakazi toka nje hata kwa yale majukumu ambayo watanzania wangeweza kufanya hususan shughuli za saluni na bustani.