Jumatatu , 18th Apr , 2022

China imeripoti vifo vya watu watatu waliofariki dunia kutokana na janga la UVIKO 19 huko jijini Shanghai ikiwa ni mara ya kwanza toka jiji hilo lilipoanza kuweka watu karantini mwishoni mwa mwezi uliopita 

Kwa mujibu wa taarifa ya tume ya afya ya nchi hiyo, waliofariki dunia ni watu wenye umri wa miaka kati ya 89 na 91na ambao walikua hawajachanjwa chanjo ya UVIKO 19. 

Mamlaka za mji wa Shanghai zinasema kuwa ni 38% pekee ya watu wenye umri juu ya miaka 60 ndio waliochanjwa chanjo hiyo . 

Jiji hilo kwa sasa linaingia tena kwenye jaribu lingine , ikiwa na maana kuwa katazo la kuonekana nje litaingia wiki ya nne sasa. 

Vifo vilivyoripotiwa leo ni vya kwanza kabisa kuthibitishwa kuwa vimetokana na janga la UVIKO 19 toka mwezi March janga hilo lilipogundulika tena jijini Shanghai. 

Tume hiyo ikitangaza vifo hivyo imesema kuwa, watu hao watatu wamefariki dunia wakiwa hosptali siku ya jumapili ya jana, na kwamba kulikua na juhudi zote za kujaribu kuokoa maisha yao. 
Taarifa hiyo imeongeza kuwa watu hao watatu walikua na matatizo mengine ya kiafya. 

Wananchi wa eneo hilo wamekua na hasira kali ya kufungiwa ndani toka wimbi la Omicron lilipoibuka jijini humo wiki tatu zilizopita , wengi wakilalamikia kuishiwa chakula