Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Chimbuko la Siku ya wanawake Duniani

Jumatano , 8th Mar , 2017

Leo tarehe 8 Machi, 2017 dunia zima inaadhimisha Siku ya Wanawake Duniani, ambayo huadhimishwa kila mwaka kwa lengo la kutambua na kuthamini mchango wa mwanamke katika jamii.

Chimbuko la kuanzishwa kwa Siku ya Wanawake lilianza mwanzoni mwa miaka ya 1900 kufuatia maandamano ya wanawake wafanyakazi wa sekta ya viwanda nchini Marekani kupinga mazingira duni ya kazi.

Waandamaji hao, walilalamikia ukosefu wa huduma za kijamii na kuwepo kwa vitendo vya unyanyasaji katika ajira ikiwemo wanawake kulipwa mshahara mdogo kwa kazi sawa ukilinganisha na wanaume.

Kwa kuzingatia hali hiyo, Umoja wa Mataifa baada kuanzishwa mwaka 1945 uliridhia kuwa tarehe 8 Machi kila mwaka iwe ni Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani.

Uamuzi wa Umoja wa Mataifa wa kuanzisha Siku ya Wanawake Duniani ulitokana na ukweli kwamba masuala ya haki, maendeleo na usawa wa wanawake yalihitaji msukumo maalumu na wa kipekee.

Maandamano ya kwanza kufanyika, ilikuwa ni mwaka 1908 nchini Marekani yakihusisha wanawake wafanyakazi kwenye sekta ya viwanda

Lengo kuu la kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani ni kutoa fursa kwa jamii kupima utekelezaji wa maazimio, matamko, mikataba na itifaki mbalimbali za Kimataifa, kikanda  na kitaifa zinazohusu masuala ya maendeleo ya jinsia na uwezeshaji wanawake.

Hii ni pamoja na kuhakikisha kuwa haki za wanawake kiuchumi, kijamii, kiutamaduni na kisiasa zinapatikana na zinalindwa.

Kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani ni kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kutambua na kuthamini uwezo na mchango mkubwa wa wanawake katika kuleta maendeleo pamoja na kuelezea jitihada mbalimbali zilizofanywa na Serikali na wadau mbalimbali katika kuwajengea uwezo wa kiuchumi na kijamii ili waweze kushiriki kikamilifu katika kujiletea maendeleo yao, familia zao, jamii na Taifa kwa ujumla.

Kwa Tanzania wanawake ni kundi kubwa na muhimu katika jamii (asilimia 51 ya Watanzania Wote) hivyo hakuna maendeleo yeyote yanayoweza kufikiwa ikiwa kundi hili litaachwa nyuma.

 

HABARI ZAIDI

Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa

Maandamano yetu sio kelele za wahuni - Golugwa

Nyumba ambayo mwili wa mwanaume ulikaa hadi kuharibika

Mke aishi na maiti ya mumewe akiamini atafufuka

Ofisa wa idara ya manunuzi na mikataba akimpatia maelezo mmoja wa wananchi wawaliojitokeza kutembelea banda la GGML katika maonesho ya OSHA na kujifunza namna kuzingatia usalama katika shughuli zao za kila siku.

GGML yaja na teknolojia za kisasa za uokoaji

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Rais Samia asema CDF mwanamke atapatikana 2030

Mratibu wa idara ya dharura (ERT) kutoka GGML, Mohamed Mwaimu akimuonesha mama lishe namna ya kuzima moto wakati inatopokea mtungi wa gesi unapopata hitilafu na kulipuka. Mafunzo hayo yametolewana GGML kwa kushirikiana na OSHA kwa akina mama lishe 50 wa mkoani Arusha.

Mama lishe wafundishwa kulikabili janga la moto