Ijumaa , 3rd Mei , 2024

Chifu Mkuu wa Kabila la Wasafwa Rocket Mwanshinga ameonya tabia za washirikina kutesa watu majumbani mwao usiku na kwamba hali hiyo iwe mwisho kuanzia sasa.

Rocket Mwashinga, Chifu Mkuu wa Kabila la Wasafwa

Chief Rocket Mwashinga ameyasema hayo katika kusanyiko la msiba wa kijana Fredrick Mashaka Mbughi lilikuwepo eneo la Isanga Jijini Mbeya leo Mei 3,2024.

Aidha, katika hatua nyingine Chief Rocket amewataka vijana kuacha mara moja kunywa vinywaji vikali ambavyo vinahatarisha maisha yao ikiwemo upungufu wa nguvu za Kiume.

Awali akizungumza katika msiba huo, Chifu Mwashinga amekemea tabia za wazazi hususani wanawake kupokea watoto wa watoto wao wa kike na kuachiwa majumbani ambapo hali hiyo inaongeza watoto wa mitaani na wasichana kuendelea kuzalia nyumbani bila hofu huku mmomonyoko wa maadili ukizidi.

Mbali na hayo, amekemea vijana wa vyama vya siasa kuanzisha fujo nyakati za uchaguzi na kwamba CCM ambacho ni chama tawala wawe wa kwanza kulinda Amani na Utulivu huku akimsimamisha Mwenyekiti wa UVCCM Mbeya Mjini Ndugu Clemence Mwandemba na kumweleza kuwa hataki kusikia vijana wa chama hicho wakianzisha fujo.