Mwenyekiti wa chama cha watu wenye ulemavu Tanzania (CHAWATA ) Hamadi Komboza
Kauli hiyo ameitoa hii leo Agosti 14, 2024, na kusema licha ya kwamba wanashukuru watu wenye ulemavu kuwepo bungeni lakini wanatamani apatikane mwakilishi kutoka CHAWATA.
"Tunashukuru kwamba wenzetu wenye ulemavu wapo bungeni lakini wale si wabunge wa watu wenye ulemavu na hili limelisema kila siku na nitaendelea kulisema kwa sababu wale wapo lakini sio kwa takwa la watu wenye ulemavu wenzetu walioko bungeni ni wawakilishi wa vyama vyao vya kisiasa kwahiyo tunahitaji kuwa na wawakilishi bungeni wanaotokana na chama cha watu wenye ulemavu," amesema Komboza