Jumatano , 12th Jul , 2023

Serikali kupitia bajeti ya mwaka 2023/2024 imepanga kuboresha mifumo ya umwagiliaji kwa wakulima wa Chato walio pembezoni mwa Ziwa Victoria kwa kuweka pampu kubwa za kuwezesha kilimo cha umwagiliaji kwa kuvuta maji kutoka ziwani kwenda kwenye mashamba yao

Wananchi wa Chato

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Kilimo, Anthony Mavunde katika viwanja vya Bwera wilayani Chato aliposhiriki zoezi la uzinduzi wa kampeni ya kapinduzi ya kilimo na uchumi wilayani Chato.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Mavunde amefurahishwa na jinsi uongozi wa wilaya ulivyojipanga na kuweka mikakati ya kufanya mapinduzi ya kilimo, na kuahidi kwamba Wizara ya Kilimo ipo tayari kuanzisha mashamba makubwa kwa ajili ya mradi wa vijana ujulikanao kama Building a Better Tommorow (BBT) ili vijana na wanawake wa Chato wanufaike na mradi huo.

Akiwa katika uzinduzi wa kampeni hiyo, Mheshimiwa Mavunde alishuhudia utiaji Saini wa mikataba ya utatu, baina ya vyama vya ushirika, Bodi ya Tumbaku na Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko na upande wa tatu ni Benki na kupongeza tukio hilo na kuwahamasisha wakulima kuongeza uzalishaji kutokana na kupatikana kwa soko la uhakika.