
Basi la kampuni ya TASHRIFF likiwa limetekea kwa moto
Mapema leo asubuhi kupitia mtandao ya kijamii kulisambaa taarifa iliyonesha moja ya mabasi ya abiria ya kampuni hiyo likitekea kwa moto katika maeneo ya Tanga mjini mkoani humo.
Akizungumza na www.eatv.tv kamanda Edward Bukombe amesema ni “ajali tu gari ilipata hitilafu gari likapata moto, mpaka dakika hii chanzo cha ajali kinaendelea kuchunguzwa, na ajali haikuwa na madhara kwa binadamu ila gari ndilo lilikuwa Linaelekea kubeba abiria".
Aidha kamanda huyo amekanusha taarifa ya kuwa gari hiyo ilikuwa imewaka moto eneo la kituo cha mafuta, na kusema kuwa gari lilikuwa likitoka kwenye eneo la kulaza magari kuelekea kituo cha mabasi yaendayo mikoani kwa ajili kuanza safari zake za kila siku.