
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe na Mgombea urais kupitia CHADEMA Tundu Lissu.
Akiongea na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Slaam Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema Freeman Mbowe amesema kwamba hata hivyo wanaipinga adhabu hiyo na watafungua kesi kwa hati ya dharura Mahakama Kuu kupinga maamuzi hayo.
Kamati Kuu ya Chadema pia imeridhia kumuunga mkono mgombea urais Zanzibar Seif Sharif Hamad kupitia chama cha ACT-Wazalendo, na wameanza mchakato wa kujitoa kwa mgombea urais wao wa Zanzibar.