Jumanne , 24th Jan , 2023

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Daniel Chongolo  amewaonya viongozi wanaolalamika kuhusu maeneo wanayopewa kufanyia kazi hali ambayo inawavunja moyo wananchi na kuwataka wajitathmini kama wanatosha katika nafasi zao

Chongolo amesema wanashangaa kuona baadhi ya viongozi wakiwemo Mawaziri, wakuu wa mikoa na baadhi ya viongozi wanalalamika  kutopewa ushirikiano na watumishi hali ambayo imekishtua chama hicho

Katibu Mkuu Chongolo ametoa onyo hilo  mapema leo Jijini Dodoma wakati wakupokelewa kwa Wajumbe wa Sekretarieti mpya ya chama cha Mapinduzi Taifa

Naye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM Sophia Mjema amewataka wasiasa kujibizana kwa hoja na lugha za staha huku akisema wananchi hawataki malumbano bali wanataka kupata Suluhu ya matatizo wanayokutana nayo mitaani