Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC Ahmedy Ally amesema kuwa mbali na mchezo wa kirafiki dhidi ya APR ya Rwanda ,wiki ya tamasha la Simba Day 2024 inataraji kuzinduliwa mkoani Morogoro kuunga mkono juhudi za serikali katika kutangaza Utalii hapa nchini.
“Lengo la mkutano huu ni kutangaza rasmi kuanza kwa Wiki ya Simba 2024 pamoja na maandalizi yote kuelekea Siku ya Simba (Simba Day). Kama mnavyojua kila mwaka tunajaribu kufanya jambo jipya ili kuongeza thamani ya jambo letu.”amesema Ahmedy Ally
Kwa upande mwingine,Mashabiki wa SImba SC wametamba kufanya vizuri kuelekea msimu wa mpya wa mashindano wa 2024-25 kutokana na usajili mkubwa waliofanya kwenye dirisha hili kubwa linaloendelea hapa nchini .