Jumapili , 18th Feb , 2018

Chama cha Mapiduzi CCM kupitia Katibu wake wa Itikadi na Uenezi na msemaji wa chama hiko Humphrey Pole Pole, kimetoa msimamo wake juu ya kifo cha mwanafunzi aliyeuawa na polisi, na watu kuinyooshea vidole serikali ya CCM.

Mwanafunzi Aqulina Akwilini Baftaha aliyeuawa na poilisi

Akizungumza na mwandishi wa www.eatv.tv  Pole Pole amesema tukio la kifo cha mwanafunzi huyo halipaswi kwenda hivi hivi, ni lazima wahusika wachukuliwe hatua kwani ni jambo ambalo lipo kinyume na sheria, na kuwataka watu wasiingize kwenye siasa kujipatia kura kwenye uchaguzi.

Siku ya Ijumaa ya tarehe 16, Februari mwaka huu, mwanafunzi  Aqulina Akwilini Baftaha aliuawa kwa kupigwa risasi na askari polisi waliokuwa wakiwatawanya wafuasi wa CHADEMA ambao wameelezwa walikuwa wakiandamana kinyume na sheria, na kumpata yeye akiwa kwenye daladala.

Tazama video hapa chini