Jumatatu , 19th Jul , 2021

Chama cha Mapinduzi (CCM), kimeshinda uchaguzi katika jimbo la Konde visiwani Zanzibar, baada ya mgombea wake Sheha Faki kujipatia kura 1,796 na kuwashinda wagombea wenzake 11.

Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Konde, Yasin Jabu Hamisi (kushoto) akimkabidhi hati ya ushindi Sheha Mpemba Faki, aliyeshinda Ubunge wa jimbo hilo

Matokeo ya uchaguzi huo yametangazwa leo Julai 19, 2021, ambapo Faki amepata kura 1,796 kati ya kura halali 5,020 zilizopigwa.

Uchaguzi huo mdogo umefanyika kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kutokea Chama cha ACT-Wazalendo Khatib Said, kufariki dunia Mei 19 mwaka huu.