Jumanne , 23rd Jun , 2015

Zoezi la uandikishwaji wapiga kura kwa njia ya mashine za Biometrick Voters Registration mkoani Arusha, laingia katika sura mpya ya baadhi ya waandikishwaji kuuza nafasi zao kwa shilingi 25,000 na 30,000.

Mwananchi wa Jijini akiwa anajiandikisha kwa mfumo wa BVR.

Mmoja wa vijana hao Hamis Juma wa kituo cha Muriet sekondari kata ya sokoni one, ameuza nafasi yake kwa Neema John kwa shilingi 30,000 kwa madai ya kupata kipato na kufidia siku yake aliyopoteza tangu usiku wa saa Nane alipofika kituoni hapo kujipanga hadi muda wa saa sita mchana bila kupata kitambulisho.

Amesema kuliko arudi nyumbani bila mboga ya watoto kwa kupoteza siku, bora auze apate fedha za kutumia na kesho yake atakayokuja ajipange kwa amani.

Naye Lameck sekeyan wa kituo cha Ebenezer, kata ya Muriet, amesema yeye ameuza nafasi yake kwa mwingine kwa shilingi 25,000, kwa sababu ni kijana anaweza kurudi kesho kujipanga upya na kupata kitambulisho.

Amesema hiyo kwake ni fursa ya kujiingizia kipato, kwa kuwa zoezi linaendelea hana wasiwasi atapata kitambulisho na kama kesho akitokea mtu mwingine atauza azidi kujiingizia fedha.