Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali, inaelezwa kwamba boti hiyo ilizama kutokana na kuzidisha uzito kutokana na idadi ya watu wengi waliopanda, ambao walikuwa wakivuka katika mto huo kwenda msibani.
Afisa Mahusiano wa Jeshi la Polisi wa eneo hilo, DSP Moses Yamu, amesema kwamba ajali hiyo imetokea katika eneo lenye kina kirefu zaidi cha mto huo, na miili 13 tayari imeshaokolewa, huku waokoaji wakiendelea kuwatafuta wengine.
Msemaji wa Gavana wa Benue wa masuala ya kijamii na kidini, Mchungaji John T. Aernyi, amesema kwamba mto huo umekuwa na matukio kama hayo mara kwa mara, na kushauri ufike wakati zichukuliwe hatua stahiki.