
Mhe. Majaliwa ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam, wakati akipokea hundi ya shilingi 263 kwa ajili ya kununulia madawati katika shule za mkoa wa Dar es salaam katika maadhimisho ya miaka 50 ya Benki kuu ya Tanzania.
Waziri mkuu amesema, fedha hizo zitaisaidia serikali kwa kiasi kikubwa kupunguza uhaba wa madawati mashuleni ambapo amewataka maofisa elimu pamoja na wakuu wa shule jijini Dar es salaam kuhakikisha kuwa pesa hizo zinatumika kwa kusudi lililopangwa na sivinginevyo.
Naye gavana wa benki kuu ya Tanzania Prof. Benno Ndulu amesema benki hiyo inatambua umuhimu wa elimu katika maendeleo ya nchi na kuwa wanaunga mkono juhudi za kuboresha elimu bora na ukuwaji wa uchumi.