Jumanne , 24th Jan , 2023

Gharama za ukarabatati wa uwanja wa ndege Iringa zimeongezeka kutoka bilioni 41 hadi kufikia bilioni 63 ambapo Naibu Waziri  wa Ujenzi  Mhandisi Godfrey Kasekenya amesema licha ya  ongezeko hilo serikali itahakikisha uwanja huo unakamilika kwa muda uliopangwa ili kuwezesha ukuaji wa uchumi

Naibu waziri amesema hayo mara baada ya kutembelea uwanja huo na kujionea namna ujenzi unavyoendelea ambapo amesema licha ya kuongezeka kwa gaharama hizo lakini mkandarasi bado yupo ndani  ya muda uliopangwa

Pia naibu waziri amesema kutokana na kiwanja hicho kuwa moja yakiwanja cha kimkakati kwa maneneo ya nyanda za juu kusini,benki ya dunia imekubali kujenga jengo la abiria

Kwa upande wake meneja wa wakala wa barabara mkoa wa iringa mhandisi DANIEL KINDOLE amesema uwanja huo utafanya kazi masaa ishirini na nne pindi utakapokamilika ili kuwezesha shuguli za kiuchumi kwa wananchi wa mikoa ya iringa na njombe