Serikali ya Tanzania imeokoa zaidi ya shilingi za kitanzania bilion 3 ambazo zingetumika kupeleka wagongwa wa moyo nje ya nchi kwa ajili ya matibabu ya ugonjwa wa moyo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ametoa takwimu hizo leo alipotembelea Hospital ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha moyo cha Jakaya Kikwete kwa lengo la kujionea namna kitengo hicho kinavyotoa hudumia kwa wagonjwa wanaofika hapo kwa lengo la kupatiwa matibabu ya moyo.
Waziri Mwalimu pia alimtembelea kiongozi wa Kanisa Katoliki jimbo la Dar es salaam muhashamu Polycap Kadinali Pengo ambaye amelazwa katika kitengo hicho cha moyo kwa matibabu na kupewa taarifa kuwa anandelea vizuri.
Mkurugenzi wa kitengo hicho JKCI Prof. Mohamed Janabi amesema kuwa hali ya Askofu Polycap Kadinali Pengo inaimarika na muda wowote anaweweza kuruhusiwa kurudi nyumbani kwake.