
Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa, John Pambalu.
Akizungumza na EATV&EA Radio Digital, leo Disemba 15, 2019, Pambalu amesema kuwa ataongoza kwa kuzingatia misingi ya taasisi ya chama chao na harakati za kudai Demokrasia ndani na hata nje ya CHADEMA.
"Wategemee uongozi wenye sura mbili, nitaongoza kwa kuhakikisha misingi ya kitaasisi ya hasa taasisi yetu ya CHADEMA ikifuata, pili wategemee kuna vita ya kiharakati zaidi vya kudai Demokrasia na Utawala Bora" amesema Pambalu.
Matokeo ya Uchaguzi huo yalitangazwa Disemba 10 mwaka huu, ambapo Pambalu alichaguliwa kwa Kura 150 sawa na asilimia 52, huku nafasi ya Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara, ilichukuliwa na Moza Mushi, na nafasi ya Makamu Mwenyekiti Zanzibar ikichukuliwa na Omar Othman Nassor.