Jumatatu , 5th Oct , 2015

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limekipongeza kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, kwa kutoa elimu kwa wasanii juu ya masuala yao ya msingi ikiwemo haki miliki na mengineyo.

Pongezi hizo zimetolewa na Afisa habari wa BASATA Bwana Artides Kwizela, na kusema kwamba ni suala zuri kukitaka kusukuma ajenda ya kurasimishwa kwa wasanii.

"Napenda kukipongeza kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, kwani mbali na kucheza muziki wa wasanii wetu wa nyumbani na kuukuza, lakini kinatoa elimu kwa wasanii kuhusu masuala mbali mbali yahusuyo haki miliki, haki shiriki, lakini vile vile kuwasaidia wasananii kulinda haki zao, big Up East Africa Radio", alisema Kwizela.

Wiki iliyopita Baraza la sanaa la Taifa (BASATA) walipost tweet ikipongeza kipindi hicho, na kusema maneno haya.