
Trent Alexander-Arnold
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 ambaye amekuwa katika klabu hiyo tangu akiwa na umri wa miaka sita mkataba wake unamalizika Juni 30 2025 na anatarajiwa kujiunga na Real Madrid.
"Baada ya miaka 20 katika Klabu ya Soka ya Liverpool sasa ni wakati wa mimi kuthibitisha kwamba nitaondoka mwishoni mwa msimu huu ni uamuzi mgumu zaidi ambao nimewahi kufanya maishani mwangu kwa urahisi" Alexander-Arnold alitangaza kwenye mitandao yake ya kijamii.
Beki huyo mzaliwa wa Liverpool amecheza mechi 352 akiifungia klabu hiyo mabao 23 tangu aanze kucheza kwa mara ya kwanza mwaka 2016 na kuisaidia Liverrpool kushinda makombe mawili ya EPL na UCL 2019