Ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya usiku katika wilaya za jijini Dar es Salaam ambapo maagizo hayo yakiwa ni utekelezaji wa ushauri kutoka kwa Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa Ambapo aliagiza kwa barabara za mwendokasi zinazosubiri mabasi kutumika ili kupunguza foleni.
“Bashungwa ametoa maelekezo kwa sababu kunabaadhi ya barabara kwa sababu mabasi bado hayajafika sasa tuangalie utaratibu wa kuingiza mabasi na kuingiza mabasi madogo kwa mfano barabara ya kutoka mbagala. Naomba niweke clear hapa sio barabara zote ni barabara ambazo bado hazijapata mabasi.” Amesema Albert. Chalamila.
Sambamba na hilo mkuu wa mkoa Ameagiza wakandarasi wote waliopewa tenda za ujenzi wa miundombunu ya serikali jijini Dar es Salaam kuhakikisha wanafanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha inakamilika mapema kabla ya mvua kuanza kunyesha na kuepuka kisingizio cha kutokamilisha miradi kwa sababu ya mvua.
Ziara hiyo ya mkuu wa mkoa inakuwa ni ziara yake ya kwanza ikiwa ametangaza ziara ya usiku ya siku tano kukagua miradi ya maendeleo katika wilaya za jiji la dar es Salaam.