Waziri wa ujenzi Mh. John Magufuli akisistiza jambo.
Akisoma bajeti ya Wizara ya Ujenzi leo Bungeni mjini Dodoma Waziri wa ujenzi Mh. John Magufuli amesema tatizo hilo litapungua ikiwemo ujenzi wa miradi mbalimbali ya barabara za juu na mradi wa ujezi wa barabara sita za kutoka Dar es Salaam-Chalinze
Mh. Magufuli amesema gharama za ujenzi huo zitafikia zaidi ya Trilion 2.3 ambapo amesema kukamilika kwa ujenzi huo kutarahisisha ukuaji wa uchumi wa nchi kwa itaruhusu magari mengi zaidi kuingia na kutoka jijini Dar es Salaam hasa maeneo ya Bandari.
Magufuli amesema kuwa barabara hiyo pia itakuwa na njia za sita ambapo pia itakuwa na njia za maroli pekee ili kurahisha usafirishaji.
Aidha Mh. Magufuli amesema kuwa mchakato wa utengenezwaji wa Daraja la Sarenda umekiwishaanza na serikali ya Korea imekubali kutoa mkopo nafuu ili kufanikisha ujenzi huo ambao utapugnuza foleni kwa kiasi kikubwa.