Jumatatu , 11th Apr , 2016

Serikali ya Tanzania ili iweze kufikia malengo ya milenia imeshauriwa kupanga bajeti zake kwa kuzingatia ongezeko la watu ambapo inakadiriwa kuwa kwa mwaka kuna zaidi ya ongezeko la watu milioni moja.

Dar es Salaam nai Mji wenye wakazi wengi kupita miji yote ya Tanzania, Hesabu ya sensa 2012 ilionyesha Dar es Salaam mmojawapo idadi ya watu 4,364,541.

Hayo yamebainishwa jana katika mkutano uliowakutanisha wadau na watetezi wa masuala ya uzazi wa mpango na idadi ya watu (TCDAA) na kuongeza kuwa maendeleo yatafikiwa pale tuu nchi itakapokuwa na watu inayoweza kuwahudumia halikadhalika kwa ngazi ya familia kuwe na watoto ambao mzazi anaweza kuwahudumia kikamilifu.

Akizungumza katika Mkutano huo mwakilishi wa Kikundi kazi cha wadau na watetezi wa uzazi wa mpango na idadi ya watu, Halima Sharifu, ametoa wito kwa serikali kuwekeza katika kundi la vijana na kusema litasaidia katika ukuaji wa Uchumi.

Bi. Halima ameongeza kuwa serikali inapaswa kuboresha mazingira bora ya Elimu, Afya na Sekta ya Ajira ikiwa ni pamoja kuhakikisha vijana waliokatika mahusiano wanaepuka kupata mimba zisizotarajiwa pamoja na kuepuka magonjwa ya maambukizi kwa njia ya ngono ikiwemo (UKIMWI).

Kwa mujibu wa Sensa ya watu na Makazi ya Mwaka 2012, idadi ya watu waliokuwa chini ya miaka 20 ni asilimia 54 huku idadi hiyo ikitajwa kuwa itaongezeka mara tatu katika kipindi cha miaka 30 ijayo.