Jumapili , 19th Jul , 2015

Michuano ya Kombe la Kagame imeendelea leo katika viwanja viwili, uwanja wa Taifa na uwanja wa Karume jijini Dar es slaam ambapo jumla ya michezo mitatu imepigwa.

Michuano ya Kombe la Kagame imeendelea leo katika viwanja viwili tofauti, uwanja wa Taifa na uwanja wa Karume jijini Dar es slaam ambapo jumla ya michezo mitatu imepigwa.

Katika uwanja wa Taifa Azam FC imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya KCCA ya Uganda katika mchezo wa kundi C, bao lililofungwa na John Bocco dakika ya 11 ya mchezo.

Awali katika uwanja huo pamepigwa mchezo mwingine wa Kundi C uliozikutanisha Adama City ya Ethiopia na Malakia ya Sudan Kusini ambapo Malakia imeibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Katika uwanja wa Karume kumeshuhudiwa mchezo mmoja wa kundi B uliozikutanisha LLB AFC ya Burundi na Heegan FC ya Somalia na mchezo huo kumalizika kwa suluhu ya bila kufungana.

Kesho kutakuwa na michezo miwili ya kundi A katika dimba la Taifa ambapo Telecom ya Djibout itakutana na Khartoum-N ya Sudan saa 8 mchana na kufuatiwa na mchezo kati ya Gor Mahia ya Kenya na KMKM ya Zanzibar.

Tags: