
Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja waliyopiga hivi karibuni
Waziri wa ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania Mh. Samweli Sita ametaja baadhi ya mapendekezo yatakayowasilishwa kwenye kikao hicho kuwa ni pamoja na hatua iliyofikiwa katika michakato mbali mbali inayoaendelea ukiwemo wa uundwaji wa shirikisho la kisiasa pamoja na mapendekezo na maombi ya nchi ya Sudani kujiunga kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Awali akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa maktaba ya Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyozinduliwa na mwenyekiti wa baraza la mawaziri wa Jumuiya hiyo Bi. Phillis Kandie Mh. Sita amesema baada ya kupatikana kwa maktaba ya jumuiya, nyaraka na kumbu kumbu zilizoko katika maeneo mbalimbali ya nchi wanachama zinatarajiwa kurejeshwa kwenye maktaba hiyo