Kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti
Ancelotti amefikisha idadi hiyo ya michezo ya ushindi baada ya kukiongoza kikosi cha Real Madrid kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya RB Leipzing mchezo uliochezwa katika Dimba la Santiago Bernabeu.
Mabao ya ushindi ya Madrid katika mchezo huo yamefungwa na Federicio Valverde dakika ya 80 na Marcos Asensio alifunga bao la pili dakika ya 90.


