Ijumaa , 15th Apr , 2022

Mashaka Mavunje (42), anayehisiwa kuwa ni jangili anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoa wa Katavi kwa kukutwa na meno ya Tembo mawili yenye uzito wa kilogramu 3.1, nyama ya Tembo kilogramu 90, silaha aina ya gobole, panga na kisu ndani ya hifadhi ya Taifa ya Katavi.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Katavi, Ali Hamad Makame

Kamanda wa polisi mkoani humo Ali Hamad Makame, amesema Jeshi la Polisi likishirikiana na Askari wa hifadhi ikiwa katika doria ya kukamata majangili ilifanikiwa kumnasa.

Akiendelea kutolea ufafanuzi sakata hilo Kamanda Makame, amesema mtuhumiwa bado anaendelea kuhojiwa ili kubaini washirika wake katika kazi hizo za ujangili.