Jumatano , 18th Dec , 2019

Mwanaume mmoja aliyetambulika kwa jina la Peter Kadama (50), kutoka nchini Uganda, anaripotiwa kumshambulia Mke wake kwa kumpiga, baada ya kumchinja Jogoo wake aliyepanga aliwe siku ya Sikukuu ya Christmas.

Jogoo anayedaiwa kuchinjwa kabla ya Sikukuu.

Ripoti inasema mwanaume huyo alimnunua kuku huyo kwa pesa ya Uganda Shilingi 15,000, kisha kumpeleka kwa Mke wake aitwaye Christine Kayendeke, na kutoa maagizo kwamba atachinjwa katika sikukuu hiyo.

Mkewe huyo alikiuka maagizo na kumchinja siku ya Jumapili ya Disemba 15,2019, ndipo Mume wake alipatwa na hasira kisha kumpiga nusura ya kumuua.

Kwa mujibu wa afisa wa mawasiliano wa eneo hilo Joseph Gadimba amesema kuwa, "Mwanaume alimpiga sana Mke wake nusura ya kutaka kumuua, Mwanamke huyo kwa sasa anapatiwa matibabu katika kituo cha Afya cha Budaka, kesi hii bado haijafika Polisi ila tumeamuru mwanaume huyo anatakiwa atimize majukumu ya kumgharamia hadi atakapopona" amesema Gadimba.

Aidha Gadimba ameongeza kuwa "Mwanamke atakapopata nafuu ndugu na wazaziwa pande zote mbili watafanya kikao ili kumaliza tofauti zao nakuwaunganisha tena wakae pamoja".

Source: Daily Monitor.