Alhamisi , 20th Mar , 2014

Mwanasheria Mkuu wa zamani wa Kenya Amos Wako amesema Katiba mpya ya Kenya imetoa fursa ya nafasi mbalimbali za uongozi wa juu kuombwa na wananchi wote wa Kenya bila ya upendeleo na waombaji kuhojiwa uwezo na sifa zao kwa uwazi huku wananchi wakiwash

Bw. Wako ambaye kwa sasa ni Seneta nchini Kenya ameyasema hayo mbele ya wajumbe wa Bunge maalum la Katiba katika semina ya bunge hilo iliyolenga kupata uzoefu wa nchi jirani ya Kenya katika kufanikisha kupata katiba yake mpya.

Hata hivyo wako amesema haikuwa kazi rahisi kwa Kenya kupata katiba hiyo mpya, kwani kuna watu walipoteza maisha, kupata vilema na wengine kufungwa, kabla ya taifa la Kenya kuamua kukaa pamoja na kuridhiana kupatikana kwa Katiba hiyo.

Pamoja na mambo mengine Bw. Wako amesema katiba ya sasa imezingatia usawa wa makundi yote kama vile ya walemavu, wanawake na vijana katika nafasi za uongozi wa kisiasa, jambo ambalo limeongeza idadi kubwa ya wawakilishi wa wananchi.