Kamanda wa Polisi mkoani Mara, Daniel Shillah
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa Polisi mkoani humo, Daniel Shillah amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia tarehe 10 ya mwezi Jnuari katika nyumba moja ya kulala wageni iliyopo Mugumu wilayani Serengeti.
Katika tukio lingine, Juma Waryoba maarufu kama (Kisangura) 27, anatafutwa na polisi kwa tuhuma za kumuua mkewe kwa kumchoma na kisu mara kadhaa mwilini kwake.
Shillah ameongeza kuwa tukio hilo limetokea wilayani Butiama ambapo mwanaume huyo anatuhumiwa kumuua mke wake kwa kuchoma na kisu na kisha kutoroka kusikojulikana huku chanzo kikitajwa kuwa ni wivu wa mapenzi.
Kamanda ametoa wito kwa wananchi wa mko wa Mara kuacha kujichukulia sheria mkononi kwani kama kuna migogoro ndani ya familia ni vizuri kuitatua kwa njia ya mazungumzo na sio kutumia nguvu, akisema kufanya hivyo ni kinyume cha sheria ya Jamuuri ya Muungano wa Tanzania.



