
Mwanamke mmoja wa Australia aliyepatikana na hatia ya kuwaua jamaa watatu wazee wa mumewe waliyetengana kwa mlo uliokuwa na uyoga wenye sumu amehukumiwa kifungo cha miaka 33 jela siku ya leo Jumatatu Septemba 8, katika mojawapo ya vifungo virefu zaidi kuwahi kutolewa kwa mwanamke nchini humo.
Hakimu mfawidhi alisema Erin Patterson hakuwahurumia wakwe zake baada ya kuwapa sehemu ya ya nyama ya Ng'ombe aina ya Wellington iliyotiwa uyoga wa wenye sumu.
Patterson alipatikana na hatia mwezi Julai kwa kumuua mama mkwe wake, Gail Patterson, baba mkwe, Donald Patterson na dadake Gail, Heather Wilkinson, katika kesi ambayo imekuwa ikifuatiliwa duniani kote na kupewa jina la mauaji ya uyoga wa Leongatha.
Baraza la majaji pia limemkuta na hatia mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 50 ya jaribio la kumuua Ian Wilkinson, mumewe Heather, ambaye alinusurika mlo wa 2023 nyumbani kwa Patterson huko Leongatha, mji wenye wakazi takriban watu 6,000, kama kilomita 135 (maili 84) kusini mashariki mwa Melbourne.
Jaji Christopher Beale amesema upangaji mkubwa wa mauaji na ukosefu wa majuto wa Patterson ulimaanisha hukumu yake inapaswa kuwa ndefu.
Ian Wilkinson, mmewe na Paterson awashukuru polisi na waendesha mashtaka waliomfikisha Patterson mbele ya sheria, pamoja na timu za madaktari zilizomtibu yeye na waathiriwa wengine.