Jumatano , 7th Aug , 2024

Jeshi la Polisi mkoa wa Manyara linamshikilia Robert Endrangoo mwenye umri wa miaka 43 ambaye alikimbia baada ya kumuua mke wake kwa kumkata na kitu chenye ncha kali shingoni huku mtoto wao wa miaka nane akishuhudia.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Manyara George Katabazi amesema jeshi hilo linaendelea na upelelezi zaidi na baada ya kukamilika atafikishwa mahakamani.

Inadaiwa Endrangoo alitekeleza unyama huo baada ya mkewe kumkataza kuvuna mahindi ya familia hiyo ambayo baba huyo hakushiriki kuyalima.