Rais Magufuli na Valentino Mlowola
Taarifa iliyotolewa leo Jumatano Machi 27, 2019 na Kurugenzi Mawasiliano ya Rais Ikulu, imemnukuu Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi kuwa uteuzi wa Dk Sambaiga umeanza Machi 23, 2019.
Dkt. Sambaiga ni mhadhiri mwandamizi, Idara ya Sosholojia ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Rukia Masasi ambaye amemaliza muda wake,” amesema Balozi Kijazi.
Pia, taarifa hiyo imeeleza Rais Magufuli anatarajia kumuapisha Balozi mteule, Valentino Mlowola, kuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba. Mlowola aliwahi kuwa Mkurugenzi wa TAKUKURU kabla ya nafasi yake kuchukuliwa na Kamishna wa Polisi Diwani Athuman.
Mlowola atakula kiapo hicho kesho Alhamisi Machi 28, 2019, Ikulu jijini Dar es Salaam, kuanzia saa 3:30 asubuhi.






