Ijumaa , 15th Apr , 2022

Mtu anayetuhumiwa kuwafyatulia risasi watu 10 kwenye kituo cha treni katika jiji la New York nchini Marekani, amenyimwa dhamana mpaka hapo atakapofunguliwa mashataka ya ugaidi.

Bw. Frank James, mwenye umri wa miaka  62, alipelekwa mahakamani siku ya jana kwa kufanya mashambulizi ya kigaidi kwenye halaiki kubwa ya watu.   

Alitiwa mbaroni baada ya msako mkali na polisi ambapo idadi ya watu walioumia kwenye tukio hilo imefikia watu 23.  

Mtuhumiwa huyo hajakana mashtaka yake, Lakini Mwanasheria wake ameomba mahakama ipate ripoti ya mtaalamu wa magonjwa ya akili.  

Mwanasheria  Breon Pearce akisoma hati ya mashataka alisema   ‘’Mtuhumiwa alifanya shambulizi kwa wana  New Yorke  majira ya asubuhi kwenye kituo cha treni’’

Endapo atakutwa na hatia, anakabiliwa na kifungo cha maisha jela.

Anatuhumiwa kuwapiga risasi watu 10 na kuwaua wengine 13, ambapo baada ya tukio hilo mtuhumiwa alikimbia huku akisahau vitambulisho muhimu ikiwemo kadi ya benki  ambayo ilikua na jina lake.  
Pia alikutwa na silaha ambayo ilinunuliwa kihalali huko Ohio     imesajiliwa kwa jina   "Frank Robert James".