Jumatatu , 8th Jul , 2024

Kijana Shedrack Yusuph Chaula mwenye umri wa miaka 24 aliyehukumiwa kifungo cha miaka miwili (2) gerezani au kulipa faini ya shilingi millioni 5 kwa kosa la kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni kwa mujibu wa kifungu cha 16 cha sheria ya makosa ya mtandaoni 2015,

 ameachiwa huru baada ya kulipa faini Kwa fedha alizochangiwa na wananchi.

Kijana Shadrack alipewa hukumu hiyo Julai 4, 2024 baada ya kupatikana na hatia ya kuchapisha taarifa uongo mitandaoni, kosa alilolifanya June 22 akiwa katika Kijiji Cha Ntokela na huku akijirekodi video akiwa anachoma picha inayomuonesha Rais wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya ilimhukumu Chaula ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Ntokela mkoani Mbeya, kutumikia kifungo hicho, baada ya kukutwa na hatia ya kuchoma picha ya Rais