
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt Faustine Ndugulile.
Dkt Ndugulile ametolea ufafanuzi huo leo Aprili 19, 2020, na kusema kuwa barakoa za aina hiyo zinaweza kutumiwa majumbani na sehemu za mikusanyiko na kwamba hizo siyo mbadala wa kunawa mikono na kuzingatia umbali kati ya mtu mmoja na mwingine.
"Barakoa za vitambaa zinapaswa kuzingatia mambo yafuatayo, kutumia vitambaa vya pamba, kutumia layers zaidi ya mbili katika utengenezaji wa barakoa hizo, kuwa na barakoa angalau mbili ili kuruhusu kufanyiwa usafi wa mara kwa mara, barakoa zifuliwe kwa maji na sabuni na kupigwa pasi" ameeleza Dkt Ndugulile.
Aidha akitolea ufafanuzi wa barakoa za N-95, Dkt Ndugulile amesema kuwa hizo zinapaswa kutumika na watoa huduma wa afya wanaohudumia wagonjwa wa COVID-19 na kwamba hazipaswi kuvaliwa mitaani, majumbani wala maofisini.
Kwa upande wa barakoa za upasuaji(surgical masks), hizi zinapaswa kuvaliwa na watumishi wa afya ambao hawatoi huduma za moja kwa moja kwa hao wagonjwa, ambapo hizi zinaweza kuvaliwa na jamii kwenye maeneo ya mikusanyiko kwa muda wa masaa 4-6.