Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege, Matanga Mbushi amesema kijana huyo ambaye anafanya kazi nchini Ufaransa amekamatwa akiwa na pipi 59 zenye uzito wa zaidi gramu 800, akizipeleka nchini Ufaransa.
"Tumemkamata mtuhumiwa akiwa na pipi 59, kati ya hizo 56 alizificha kwenye soksi na tatu amezitoa leo kwa njia ya haja kubwa. Yupo chini ya uangalizi maalumu,” amesema Mbushi.
Jeshi la Polisi limesema watu wachukue tahadhari wapofanya vitendo hivyo vya uhalifu kupitia viwanja vya ndege vya Tanzania, kwani serikali iko macho ikiwaangalia kwa ulinzi mkalai.



