Jumamosi , 2nd Jul , 2022

Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt. Pindi Chana, amesema mradi wa kuboresha usimamizi wa maliasili na kukuza utalii Kusini mwa Tanzania unatarajiwa kutoa ajira zaidi ya 40,000 kwa wakulima na wananchi wanaoishi kando kando ya hifadhi za Taifa.

Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt. Pindi Chana

Hayo ameyasema mkoani Iringa na kuongeza mradi huo unalenga kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea hifadhi za Taifa, vivutio vya kiutamaduni na mambo kale nchini na kwamba kupitia wizara na mradi wake wa huo utatekeleza hayo.

“Utekelezaji wa mfumo huu unategemea kwa kiasi kikubwa ushirikiano wetu kama wadau wakuu katika utekelezaji wa mradi wa REGROW, hivyo ninaomba tuutangaze mfumo huu na kuutumia kuwasilisha maoni na malalamiko yatakayotokana na utekelezaji wa mradi,” amesema Balozi Dkt. Chana.