Jumamosi , 1st Feb , 2025

Watu watatu wamefariki dunia papo hapo baada ya gari aina ya Toyota Rav4 waliokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na basi la abiria la Kampuni ya Ester Kuxury, mkoani Kilimanjaro leo Jumamosi Februari mosi, 2025

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji mkoani Kilimanjaro, Jeremiah Mkomagi amesema ajali hiyo imetokea eneo la Mdawi, Wilaya ya Moshi. 

Amesema chanzo cha ajali ni baada ya dereva wa gari dogo kuyapita magari mengine bila kuchukua tahadhari na kwenda kugongana uso kwa uso na basi hilo.

Hakuna majeruhi kwenye basi hilo, na miili ya marehemu waliokuwa kwenye gari dogo imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro, Mawenzi