Baadhi ya mashuhuda katika eneo la tukio waki
Watu 17 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 45 wamejeruhiwa katika ajali ya barabarani baada ya basi la kampuni ya Moro Best kugongana uso kwa uso na lori lililokuwa limesheheni mabomba ya maji, katika eneo la pandambili wilayani Kongwa, mkoani Dodoma.
Basi hilo lilikuwa likitokea wilayani Mpwapwa mkoa wa Dodoma kwenda jijini Dar es salaam wakati lori lilikuwa likitokea Morogoro kwenda Dodoma.
Hotmix imefika katika eneo la tukio na kushuhudia basi hilo lenye namba za usajili T258 AHV aina ya scania pamoja na lori lenye namba za usajili T 820 CQU likiwa na trela lenye namba T 390 CKT yakiwa yameharibika vibaya,
Mashuhuda wanasema kuwa ajali hiyo ilitokea wakati lori likijaribu kulipita lori lingine na likiwa kwenye mwendo wa kasi na mbele yake lilitokea basi ambapo dereva wa lori alishindwa kulimudu na kugongana uso kwa uso na basi hilo.
Majeruhi wa ajali hiyo wamekimbizwa katika hospitali ya rufaa ya Dodoma ambapo mganga mkuu wa mkoa wa dodoma Ezekiel Mpuya amethibitisha kupokea majeruhi 22 hosipitalini hapo, huku majeruhi wengine 20 wakipelekwa hosipitali ya wilaya ya kongwa.
Kamanda wa polisi mkoa wa dodoma david misime anathibitisha kutokea kwa ajali hiyo huku jeshi la polisi likiendelea kufanya uchunguzi wa kitaalamu kujua nini chanzo na kiini cha ajali hiyo