
Wanajeshi wanne wa Australia wanadhaniwa kuwa wamekufa baada yaHelkopta ya MRH-90 Taipan kutumbukia baharini wakati wa mazoezi ya kijeshi ya kimataifa siku ya Ijumaa.
Helikopta hiyo ilianguka karibu na visiwa vya Whitsunday wakati wa zoezi la Talisman Sabre - operesheni kubwa ya mafunzo ambayo kila baada ya miaka miwili hukusanya wanajeshi 30,000 kutoka Australia, Marekani na mataifa mengine kadhaa.
Lakini siku ya Jumatatu waziri wa ulinzi alisema kuwa hakuna tena matumaini ya kuwarejesha wakiwa hai, baada ya chama cha upekuzi kupata vifusi vinavyoendana na tukio aliloliita la kutisha.
Siku ya Alhamisi, mratibu wa utafutaji alitangaza eneo jingine la vifusi - wakati huu ikiwa ni pamoja na sehemu kubwa zamabaki zilipatikana mita 40 chini ya uso wa bahari.Gari lililokuwa likiendeshwa kwa mbali pia lilipata mabaki ya binadamu ambayo hayakutambuliwa.
Mamlaka zilianzisha msako wa kuwatafuta askari waliopotea ndani ya ndege hiyo wote kutoka kwa Kikosi cha Sita cha Anga.