Jumatatu , 29th Jan , 2024

Afisa Mkuu wa masuala ya fedha (CFO) kutoka Kampuni ya AngloGold Ashanti inayomiliki Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML), Gillian Doran wiki iliyopita alikaribishwa na kuutembelea mgodi huo uliopo mkoani Geita.

2. Zulu Nkanyiso, Meneja Mwandamizi wa Mtambo wa uchenjuaji akijibu maswali kutoka kwa Gillian Doran, Afisa Mkuu wa Fedha wa AngloGold Ashanti, kuhusu muongozo wa GGML wa usimamizi na uhifadhi wa takasumu (TSF). Pia walikuwepo Gilbert Chamlonde, Meneja wa Uchimbaji wa kina kifupi juu ya ardhi (kushoto). Kutoka kulia kwenda kushoto: Yusuph Mhando, Meneja Mazingira; Ikingo Gombo, Meneja Mwandamizi – Masuala ya fedha & Mnyororo wa ugavi na Godvictor Lyimo, Meneja Mwandamizi - Utatuzi wa Migogoro ya Kodi.

Mbali na Doran pia Meneja Mwandamizi wa Ushuru – Afrika, Jacques Labuschagne na Makamu wa Rais wa masuala ya Fedha – Afrika, Himesh Persotam pia waliitembelea GGML.

Ziara yao haikuwa ya kihistoria tu, kwani ilikuwa ni ziara ya kwanza ya CFO, lakini pia ilitoa maelekezo muhimu kuhusu shughuli za mgodi huo wa dhahabu wa Geita.

Gillian Doran, Afisa Mkuu wa Fedha wa AngloGold Ashanti (katikati), pamoja na Himesh Persotam (mwisho kushoto), Makamu wa Rais: Masuala ya Fedha - Afrika, na Jacques Labuschagne, Meneja Mwandamizi wa masuala ya Ushuru Afrika, (wa pili kutoka kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja kando ya mgodi wa Nyamulilima na baadhi ya menejiment ya GGML.