Mtumiaji huyo wa mtandao wa TikTok anayetumia jina la M.Mojela aliweka video hiyo mwanzoni mwa wiki hii ikimuonyesha akipiga goti moja ishara ya kumuomba mpenzi wake akubali kuvishwa pete huku msichana huyo akilia.
Katika tukio hilo Jeneza la baba wa msichana huyo linaonekana likiwa umbali wa mita moja kutoka alikopiga goti mwanaume huyo.
Watumiaji wa mitandao ya kijamii nchini Afrika kusini wameonyesha kuwa na mawazo tofauti kuhusu tukio hilo huku wengine wakikosoa kitendo hicho.
Bado haakuna mwanafamilia aliyejitokeza kufafanua kuhusu tukio hilo la aina yake la mwanaume kumvisha pete mchumba wake katika msiba wa baba yake