
Anord Mpobela, aliyechomwa kisu
Tukio hilo limetokea siku ya Tarehe Tisa mwezi mei mwaka 2023 majira ya Mchana katika eneo la barabara inayopandisha mtaa wa Jogoo house jijini Arusha,ambapo tayari Mhanga wa Tukio hilo amekwisha wasilisha taarifa hizo kwa jeshi la polisi kwa hatua za kisheria zaidi.
Akizungumza Mchungaji huyo amesema kwamba,"Kwenye habari ya kuchomwa kisu ni lazima niwe na tahadhari kwa sababu sijajua kile kisu kilikuwa na sumu gani, naiomba serikali ituangalie wahubiri wa injili na kwa sababu serikali yetu haina udini, ningefurahi kuona tunapewa ulinzi na vibali vya kuhubiri injili vikatoka kwa wakati sio kuzungushwa,".
Mmoja wa watumishi wa kanisa hilo, amelalamikia uwepo wa changamoto wanayoipata hasa wanapokuwa wakihubiri injili mitaani na kuiomba serikali waitambue kazi yao kwani inao umuhimu katika ustawi wa Taifa.