Jumatatu , 10th Jan , 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amesema kwamba hakuwarudisha tena kwenye Baraza la Mawaziri aliloliteua juzi, wabunge William Lukuvi na Profesa Palamagamba Kabudi, kwa sababu kawapa kazi maalum Ikulu hivyo atakuwa nao.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Kauli hiyo ameitoa hii leo Januari 10, 2022, mara baada ya kuwaapisha Mawaziri, Manaibu Waziri, Makatibu Wakuu na Makatibu Wakuu wasaidizi Ikulu ya Chamwino Dodoma, na amewachukua hao wawili kwa lengo la kuwasimamia viongozi wengine kwani tayari wao wameshafikia umri wa kustaafu.

"Kaka yangu Lukuvi ana kazi na mimi, nimeona meseji nyingi nyingi, afadhali Lukuvi ametoka, hajatoka yupo, wengine wameanza kumletea meseji za ajabu wakijua atagombania Uspika, hatagombania ana kazi na mimi, msianze kumchafua, ametumikia Taifa hili kwa uadilifu, mwache aende na mimi tumalize kazi," amesema Rais Samia