Alhamisi , 3rd Dec , 2015

Kampuni ya Madini ya ACACIA, inayomilikia migodi mitatu ya dhahabu ikiwemo Buzwagi, North Mara na Bulyanhulu imeanza zoezi la kupunguza wafanyakazi wake ili kukabiliana na athari za kushuka kwa soko la dhahabu katika soko la dunia.

Meneja Mkuu wa rasilimali watu wa kampuni hiyo Bi. Janet Lekashingo

Akizungumza Jijini Dar es Salaam Meneja Mkuu wa rasilimali watu wa kampuni hiyo Bi. Janet Lekashingo amesema kuwa kwa kipindi cha miaka miwili, bei ya dhahabu ilianza kupungua kwa kasi hivyo kutishia uhai wa uzalishaji wa madini hayo.

Aidha Bi. Janet ameongeza kuwa bei ya dhahabu ilishuka mpaka kufikia dola 1100 kwa wakiwa, hivyo kampuni imeona haina budi kupunguza wafanyakazi kwa kuangalia uchambuzi wa kazi muhimu zinazoweza kufanyika na watu wachache katika uzalishaji.

Ameongeza kuwa zoezi hilo linaweza kuwakumba zaidi ya wafanyakazi elfu moja wa kampuni hiyo lakini pia wanaendelea na mchakato wa kubana matumizi katika sehemu nyingine ambazo hazina umuhimu katika uzalishaji.