Jumatatu , 27th Apr , 2015

Kiwanda cha A to Z kupitia kituo chake cha utafiti cha Afrika ATRC, kimegundua teknolojia mpya ya kuhifadhi nafaka kwa kutumia mifuko imara inayohifadhi nafaka hizo kwa kipindi kirefu bila kutumia dawa yoyote.

Mkurugenzi wa kituo cha utafiti wa magonjwa ya wadudu Dkt, Johnson Ouma kwa kwanza kulia,

Ugunduzi wa teknolojia hiyo umeelezwa utaokoa zaidi ya shilingi Milioni 800 za wakulima zinazozawadiwa kupotea katika kila msimu wa mavuno baada ya wadudu kuingia kwenye mifuko hiyo itakayoanza kuzalishwa hivi karibuni.

Mkurugenzi wa kituo hicho Dkt, Johnson Ouma amesema suluhu ya upotevu mkubwa wa mazao kwa kutobolewa na wadudu imepatikana na hivyo kuwataka wakulima kuwa tayari kupokea mifuko hiyo.

Dkt Ouma amesema mfuko huo uliotengenezwa kwa kutumia teknolojia ya Agro Z bag Plus ni wa kwanza nchini na kwamba katika majaribio waliyoyafanya mfuko huo una uwezo mkubwa wa kuhifadhi nafaka mbalimbali.

Ameongeza kuwa kituo hicho cha utafiti wa magonjwa ya wadudu Afrika, kiliamua kufanya utafiti wa nama ya kuhifadhi mazoa kufuatia wakulima wa Tanzania kupoteza zaidi ya sh. Bilioni 800 kwa mwaka.