JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kukamata watuhumiwa 1,065 kwa makosa mbalimbali yakiwemo makosa ya unyang’anyi kwa kutumia nguvu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina wa Polisi Kanda Maalum, Simon Sirro amesema kuwa watuhumiwa 1,065 walikamatwa katika operesheni inayofanywa na jeshi hilo.
Amewataja watuhumiwa hao ni wapiga debe katika sehemu mbalimbali za vituo vya daladala, watengenezaji pombe haramu ya Gongo waliokamatwa na lita 952 ikiwemo na mitambo mitatu ya kutengezea pombe hiyo, Kikosi cha mbwa mwitu 10, wauzaji na wavutaji bhangi puli 277, Kete 210, misokoto 144, pamoja na wacheza kamari.
Kamanda Sirro amesema katika operesheni ya Julai 21 wameweza kufanikiwa kupata silaha aina ya gobore yenye namba za usajili HD 201-2014 kutoka kwa watuhumiwa wanaotumia silaha katika matukio ya uhalifu iliyotelekezwa na watu wasiofahamika baada ya raia wema kuhisi kuna mtu anamiliki silaha na msako ukaendelea.
Aidha amesema mnamo Juni 16 hadi 19 Polisi wamemkamata lita 952 za Gongo katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam kati ya lita hizo 420 zilikamatwa katika maeneo ya Kinzudi Wazo Hill kutoka kwa watu sita, mitambo mitatu ya kutengeneza pombe haramu ya Gongo pamoja na kukamata sukari kilo 100.