Alhamisi , 7th Apr , 2022

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Profesa Abel Makubi amesema kuwa takwimu zinaonesha wananchi wanaokutwa na maradhi ya saratani wamefikia 40,000 kila mwaka nchini.

Makubi amesema idadi hiyo ni kwa wale ambao wamegundulika kutokana na kuwa katika hali mbaya kiafya huku akishauri watanzania kuwa na tabia ya kufanya vipimo kwa mwaka mara moja au kila baada ya miezi sita

Kauli hiyo ameitoa wakati wa kongamano la nane la Sayansi kuhusu matokeo ya utafiti wa saratani ya damu, lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi (MUHAS). 

Aidha ameweka wazi kuwa dalili za saratani ziko nyingi kwa hiyo wananchi wasipuuze dalili zozote za ugonjwa au kutojisikia vizuri kiafya.

“Dalili za kansa zipo nyingi, unaweza kupungua uzito, kujisikia homa, kupungikiwa damu au kukohoa damu na matatizo ya tumbo kwa kansa ya tumbo kwa hiyo wananchi wanapojisikia hawako sawa kiafya ni vizuri kwenda kupima mapema”, amesema Makubi.