Jumanne , 12th Jul , 2022

Wanawake Wajasiriamali zaidi ya 100 waliokuwa wanafanya biashara ndogo ndogo za kuuza mboga mboga, matunda na Samaki katika soko la Mwanga Manispaa ya Kigoma Ujiji, wamelalamikia uongozi wa Manispaa hiyo kwa kukosa nafasi katika soko jipya

Wamesema tangu wamesimama kufanya biashara baada ya soko la Mwanga kuvunjwa ili kupisha ujenzi wa soko la kisasa, bidhaa zao walizohifadhi nyumbani zimeharibika kwa kuoza kwa kukosa sehemu ya kuuzia.

Wameeleza kuwa kila siku wanashinda katika soko jipya lililoko eneo la Masanga Jirani na stendi kuu ya mabasi kusubiri viongozi wawagawie maeneo lakini wamekuwa wakiwakwepa.

Akizugumzia suala hilo Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango Miji wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kitongoni Himid Omary, amesema malalamiko ya wanawake hao yatawasilishwa kwa timu iliyoundwa ya halmashauri kwa ajili ya kushughulikia ugawaji wa maeneo.